4/26/16

Aliyevumbua “Please Call Me” ashinda kesi


Huduma hiyo ilianza kutumiwa mwaka 2001

Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini imeiamuru kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kumlipa mwanamume aliyebuni wazo la kutuma ujumbe wa kumuomba apigiwe simu.

Gazeti la Sowetan la Afrika Kusini linasema mwajiri wa zamani wa Vodacom Nkosana Makate aliambia mahakama kwamba huduma ya "please call me" ilitokana na wazo lake.

Huduma hiyo humuwezesha anayetumia simu kutuma ujumbe bila malipo kwa wateja wengine akiwaomba wampigie simu.

Tovuti ya Tech Central ya Afrika Kusini inasema uamuzi wa kesi hiyo, ambayo imesikizwa tangu 10, itakuwa na athari kubwa.

Haijabainika Bw Makate atalipwa pesa ngapi na Vodacom.

Lakini awali amewahi kuambia Moneyweb kwamba uvumbuzi huo wake ulizalishia kampuni hiyo karibu randi 70 bilioni za Afrika Kusini ($5bn; £3bn) na alitaka alipwe 15% ya pesa hizo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts