4/26/16

Bangi ekari Tatu Yateketezwa

Polisi wilayani Kilindi, Mkoa wa Tanga imeteketeza shamba la ukubwa wa ekari tatu lililokuwa limepandwa bangi katika Kijiji cha Mkonde.


Ofisa wa Dawati la Jinsia wa jeshi hilo wilayani Kilindi, Fadhila Kiula amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya dawa za kulevya na mimba za utotoni kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2016, George Mbijima.


Amesema bangi hiyo ilikuwa imepandwa kwa kificho katikati ya mazao ya mahindi na maharage, jambo ambalo lilikuwa ni vigumu kujua haraka, lakini wananchi wenye nia njema walitoa taarifa za siri.


“Baada ya kupata taarifa hizo za siri, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na viongozi na wananchi liliweza kuteketeza bangi yote shambani hapo kwa moto na kumkamata mmliki wa shamba hilo na amefikishwa mahakamani,” amesema Fadhila.
 
MWANANCHI
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts