4/23/16

Bilioni 1.3 Zapatikana Kwenye Mnada wa Tanzanite

 

SERIKALI imepata zaidi ya Sh bilioni 1.3 katika mnada wa madini aina ya tanzanite yaliyokamatwa na kutaifishwa.

Mnada huo ulifanyika juzi wakati wa maonesho ya tano ya Kimataifa ya madini ya vito na usonara jijini hapa na kusimamiwa na Mkurugenzi wa Uthaminishaji wa Almasi na Vito kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Archard Karugendo.Mnada mwingine uliofanyika katika maonesho hayo ulikuwa ni wa madini ya tanzanite kutoka mgodi wa TanzaniteOne na Stamico, madini ambayo yalikuwa hayajakatwa na yaliuzwa kwa zaidi ya Dola za Marekani milioni 2.2 (sawa na Sh bilioni 4.6). Karugendo alisema katika mauzo hayo ya madini ya Tanzanite One, Serikali imepata mrabaha wa zaidi ya Sh milioni 245.

“Katika fedha hizo zilizopatikana kutokana na mauzo ya Tanzanite kutoka mgodi wa TanzaniteOne, serikali itapata mrabaha wa zaidi ya Sh milioni 245 na matokeo ya mauzo ya maonesho yote yatatangazwa na kamati ya maandalizi ila haya ni matokeo ya madini yaliyouzwa kwenye mnada tu,” alisema Karugendo Kaimu Kamishna wa Madini kutoka wizara hiyo, Ally Samaje alisema mapato hayo yaliyotokana na mnada huo yanakwenda moja kwa moja serikalini.

“Mapato yote hayo zaidi ya Sh bilioni 1.3 yanaingia serikalini, kwani madini hayo yalikamatwa na kutaifishwa na yalikuwa chini ya serikali tangu mwaka jana yalipokamatwa, “ alisema Samaje.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts