4/23/16

Chadema Yamtumbua Magufuli, Prof. Shivji, Prof. Bana

 Dk. Vicent Mashinji, Katibu mkuu wa Chadema akihutubia kongamano la Chaso, Mkoa wa Dodoma

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema, Rais Dk. John Magufuli ni mkwapuaji.

Kimeeleza, Rais Magufuli amekwapua sera za chama hicho kwa pupa lakini hana uwezo wa kuzitekeleza kwa kiwango kinachokubalika.

Pia kimeeleza, Rais Magufuli anatokana na chama chenye misingi ya wizi na kwamba, serikali yake chini ya uongozi wa (CCM) haiwezi kuwa na safi.Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma na Katibu Mkuu wa chama hicho Taifa Dk. Vicent Mashinji, wakati akifungua kongamano la Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) na Umoja wa Wanachadema Vyuo Vikuu (CHASO).

Katika hotuba yake Dk. Mashinji amedai kuwa, Rais Magufuli amekuwa akifanya maigizo ya utumbuaji majipu kwa baadhi ya watumishi ili kuwaaminisha Watanzania kwamba kazi anayoifanya ni sahihi.

Hata hivyo amesema, Chadema hawapingi utumbuaji wa majipu na kwamba ni lazima utumbuaji huo ufuate sheria na kanuni za utumishi wa umma.

“Nawakumbusha masuala ya haki, hakuna haki bila wajibu. Watawala wanatuongelea sisi, mbona wao hawajiongelei, kwetu sisi wajibu wao ni kufuata kanuni za nchi. Hivi hawa Mawaziri wamefanya kazi gani mpaka sasa,’’amehoji Dk. Mashinji.

Dk. Mashinji amesema, kwa sasa tatizo kubwa lililopo nchini ni mfumo uliowekwa na viongozi waliopita ambao wengi walikuwa wala rushwa.

“Tatizo la rushwa ni mfumo, ukiona mmoja katajwa ujue kuna 100 wapo nyuma yake. Hata hili la kuazishwa Mahakama ya Mafisadi limewahi kufanywa mwaka 1983 lakini halijasaidia,’’ amesema.

Mwanahalisi

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm