China, Tanzania kujenga reli ya kati | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

4/25/16

China, Tanzania kujenga reli ya kati
Rais John Magufuli

Dar es Salaam. China imekubali kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,561 kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ambao zabuni za ujenzi zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.
Balozi wa China hapa nchini Dk Lu Youqing ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli ambapo pia amemkabidhi barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa China, Xi Jinping.
Katika Mazungumzo hayo Dk Magufuli amemweleza Balozi Lu kuwa Tanzania imedhamiria kuanza ujenzi wa reli ya kati haraka iwezekanavyo na tayari imetenga fedha kiasi cha Sh 1 trilioni katika bajeti yake ijayo kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi huo.

google+

linkedin