4/23/16

CWT yawazawadia mabati wastaafu


 
Chama Cha Walimu nchini (CWT) katika Manispaa ya Dodoma, jana, kilikabidhi mabati 180 yenye thamani ya Sh3 milioni kwa walimu wastaafu tisa, ikiwa ni mkono wa heri kutokana na utumishi wao.
Mwenyekiti wa CWT wa manispaa hiyo, Samuel Mkotya alisema zawadi hiyo ni mwendelezo wa mpango wao wa kuwakumbuka walimu wanaostaafu na waliopewa ni wastaafu wa kati ya Julai na Desemba, 2015.
“CWT inawapa mkono wa pole, nendeni mkaendeleze makazi yenu baada ya kumaliza utumishi wenu, tunawashukuruni sana katika utumishi uliotukuka,” alisema Mkotya.
Mmoja wa wastaafu hao, Martha Dande alisema licha ya msaada huo kuwa mzuri, walipaswa kuulizwa wanachotaka.
Alisema kuwapa mabati ni sawa na kuwataka kujenga katika shule walizokuwa wanafundisha wakati wengine wanatoka mikoa ya mbali ambako yatahitaji nauli kubwa kuyafikisha.
Kwa upande wake, Reya Mgonho alisema wastaafu wanakabiliwa na changamoto ya kucheleweshewa mafao baada ya kustaafu.
Alitoa mfano kuwa, tangu astaafu Novemba mwaka jana hajalipwa hata nauli ya kurudi kwao. 
 
chanzo: Mwananchi
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm