Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

4/22/16

Daraja la Kigamboni laibua mjadala mzito Z’bar

BAADA ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Aboud Jumbe, kuishi kwa zaidi ya miaka 32 katika mji mdogo wa Kigamboni,..
Baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Zanzibar wamesema haikuwa muafaka kwa Daraja la Kigamboni kutotumika kwa jina lake kama mchango wa kumuenzi kutokana na historia ya maisha yake ya kisiasa kuishia katika mji huo.
Akitoa hoja hiyo mjini Zanzibar jana, Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni, Jaku Hashim Ayoub, alisema ni jambo la kushangaza kwa daraja hilo kupendekezwa kupewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye hakuwahi kuishi Kigamboni.
“Zanzibar imekuwa mfano katika kuwaenzi viongozi wa kitaifa kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa, ndio maana kuna Barabara ya Benjamin Mkapa, Nyerere Road, Chuo cha Mwalimu Nyerere, Kawawa na viongozi wengine wa kimataifa akiwamo Haile Selassie, Ben Bella, sasa kuna ubaya gani daraja lile likapewa jina lake ambalo linafanana na mji huo wa Kigamboni?” alihoji Hashim Ayoub.
Alisema historia ya Mzee Aboud Jumbe ni kubwa katika siasa za Tanzania kutokana na nafasi alizowahi kushika na maisha yake ya kisiasa yalivyoishia katika mji huo na hatua ya kulipa daraja jina lake ni kumbukumbu moja kubwa ya maisha ambayo ingeendelea kubakia kwa Watanzania.
Mwanaharakati maarufu wa Zanzibar Ali Makame Issa, alisema Watanzania lazima wajenge utamaduni wa kuwaenzi viongozi wa kitaifa waliotoa mchango mkubwa katika kutumikia taifa, lakini pia kuangalia na historia pamoja na mazingira halisi ya eneo la Kigamboni ambalo lina hostoria kubwa na maisha ya Mzee Jumbe.
Hata hivyo, alisema hakuna sababu kwa Wazanzibari kunung’unika kwa vile Zanzibar yenyewe ndio ilitakiwa ioneshe mfano kwa kumtafutia kitu kikubwa cha kumuenzi Jumbe, kwa sababu ndiye aliyefanya kazi kubwa ya kujenga demokrasia na utawala bora.
Alisema Mzee Jumbe ndiye mwanzilishi wa Baraza la Wawakilishi na kuunda Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, hatua ambayo ilifungua mlango wa demokrasia pamoja na kuwapa nafasi wananchi kutunga sheria kupitia wawakilishi wao badala ya viongozi kufanya kazi hiyo kupitia Baraza la Mapinduzi.
“Kama Zanzibar inajenga bandari huru, waanze kufikiria jina la Jumbe hatua ya kulalamikia Daraja la Kigamboni haitotusaidia kwa sababu ndio tayari lishawekwa jina, ingawa sio msahafu kusema haliwezi kuondolewa na kubadilishwa,” alisema Ali Makame Issa.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Juma Sanani, alisema pamoja na fikra ya kujengwa daraja la kigamboni chimbuko lake limetokana na Mwalimu Nyerere, lakini awamu zilizopita hazikutekeleza haikuwa vibaya kupewa jina lake.
Hata hivyo alisema kama historia imetengenezwa na kupewa jina daraja hilo la Mwalimu Nyerere, Mzee Jumbe atakuwa hakutendewa haki kwa jina lake kutozingatiwa wakati yeye ni mkazi wa Kigamboni kwa miaka mingi kati ya viongozi wa kitaifa wanaoishi katika mji huo.
Naye Ashura Said Hassan mkazi wa Mkunazini alisema jina la Nyerere katika daraja hilo liangaliwe upya ikiwezekana lifutwe na liwekwe la Mzee Aboud Jumbe katika kumuenzi kiongozi huyo aliyetumia nusu ya maisha yake katika mji wa Kigamboni.
Alisema kwamba Mwalimu Nyerere ameshaenziwa katika maeneo mengi ikiwamo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Uwanja wa Kambarage, barabara na minara ya Mwalimu Dodoma, Tabora na maeneo mengine, hivyo Mzee Jumbe alikuwa na kila sababu na sifa za jina lake kupewa daraja hilo.