Dk Ndalichako: Toeni Taarifa za Walimu Watoro | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

4/28/16

Dk Ndalichako: Toeni Taarifa za Walimu Watoro

Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dk Joyce Ndalichako amewataka wadhibiti ubora wa Elimu nchini kutoa taarifa za walimu watoro katika ngazi za juu iili wizara husika iweze kuwachukulia hatua.


Waziri Ndalichako aliitoa kauli hiyo jana wakati alifupokuwa akifungua mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyo fanyika katika chuo cha walimu Kleruu mkoani hapa.


Mafunzo hayo yaliojumuisha mikoa sita ya nyanda za juu kusini ambayo ni Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya huku lengo la mafunzo hayo likiwa ni uhakiki wa ubora wa KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu).


Akizungumza kwenye uzinduzi huo Dk Ndalichako alisema serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Dk John Magufuli imepania kukuza ubora wa elimu inayotolewa hapa nchini hivyo lazima iboreshwe ili kiwango cha ufaulu kiweze kuongezeka.

google+

linkedin