4/23/16

Hizi Hapa Sababu za China Kupiga Marufuku Huduma za Kampuni ya APPLE

 APPLE 1

Nchi nyingi duniani zimeridhia kupitisha Sheria ya Makosa ya Mtandao lengo kuu likiwa ni udhibiti wa uhalifu mitandaoni na kuendelea kuboreshwa teknolojia kadri inavyoendelea kukua na kubadilika.

Nchini Tanzania Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015 iliibua mijadala huku ikipingwa na wamiliki wa wadau wa masuala ya habari wakidai inawakandamiza katika kifungu cha 7(2b) kinachosema Mpokeaji wa Ujumbe anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa jinai. Mfano mtu akikutumia ujumbe aliotumiwa na wewe ukaupokea na wewe uliyeupokea utakuwa umefanya kosa la jinai.

Wadau wa Vyombo vya Habari na Wanaharakati walipaza sauti zao juu ya uwepo wa sheria hii ambavyo kimsingi inalenga kufifisha uhuru wa kutoa na kupokea habari kama ambavyo vifungu vya 31 mpaka 35 na 39 mpaka 45 vikielekeza kuwa mmiliki wa mtandao wa kijamii au mtoa huduma, pale anapobaini kosa na akalitoa na akawa kwenye mkakati wa kuitaarifu mamlaka husika, askari nae anaweza kwa wakati huohuo akaamuru kumkagua na hata kuchukua vifaa vya mwandishi wa mtandaoni ama mmiliki wa kituo cha utoaji wa habari ili kufanya ukaguzi bila amri ya mahakama.

Wakati hali ikisalia hivyo Tanzania, leo hii China imezifunga huduma za kampuni ya Apple katika mtandao pamoja na zile za filamu katika harakati ya kuweka sheria kali zitakazosimamia kile kitakachochapishwa mtandaoni.

Sheria zilizotolewa mwezi Machi mwaka jana zinakataza umiliki wa kigeni katika huduma za uchapishaji katika mitandao.

Sheria hizo pia zinahitaji kwamba kile kitakachowekwa kwenye mitandao au kurushwa hewani kama filamu iwe kwa manufaa ya raia wa China kupitia huduma za China.

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm