4/22/16

Kifo cha Prince chabainika, alitumia madaya ya kulevya kumzidi


Msanii Prince alikuwa akitibiwa kutokana na kutumia madawa ya kulevya kupitiliza siku sita kabla ya kifo chake, TMZ wameandika.Kwa mujibu wa tovuti hiyo, ndege binafsi ya Prince ilitua kwa dharura huko Moline, Illinois Ijumaa iliyopita, saa chache baada ya kutumbuiza Atlanta.

Kipindi hicho wawakilishi wake walidai kuwa alikuwa akisumbuliwa na mafua, kitu ambacho kilizua maswali kwasababu ndege yake ilikuwa imebakiza dakika 48 tu kufika nyumbani kabla ya kuamua kutua kwa dharura.

Vyanzo mbalimbali kutoka Moline vimeuambia mtandao huo kuwa Prince aliwahishwa hospitali na kupewe huduma ya haraka (save shot) kumsaidia.

Vyanzo hivyo vimedai kuwa madaktari walimshauri Prince akae hospitali hapo kwa saa 24. Watu wake walitaka chumba binafsi na walipoambiwa kuwa haiwezekani, Prince na wenzake waligoma.

Muimbaji huyo aliondoka saa tatu baada ya kufika hapo na kuelekea nyumbani. Vyanzo hivyo vimedai kuwa Prince aliondoka akiwa hajisikii vizuri.

Prince alikutwa hajitambui jana kwenye lifti kabla ya kutangazwa kuwa amefariki.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts