4/27/16

Kikao cha Dharura cha Baraza Kuu la COTWU, Chawasimamiska uongozi Mwenyekiti na Katibu wake Taifa
Kikao cha Baraza kuu la dharura la Chama cha wafanyakazi wa mawasiliano na Uchukuzi (COTWU),kimewasimamisha uongozi mwenyekiti na katibu wake wa Taifa, kufutia tuhuma kadhaa ikiwemo matumizi mabaya ya Ofisi.

Kikao hicho kilichofikia maamuzi hayo,kwa mujibu wa katiba yake kifungu nambari 4.2,kimefanyika jijini Dar e Salaam, na kuwakutanisha wenyeviti wa kanda Tano za Chama hicho ambapo mwenyekiti wa kanda ya Dar Es Salaam,GEORGE FAUSTIN, amesema,uamuzi wa kuwa na kikao hicho cha dharura,unafuatia alichodai makandokando mengi ya uongozi wa juu wa chama hicho ikiwemo kuongozwa na watu ambao aidha wamestaafu ama kutokuwa tena kazini.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kanda ya Dar Es Salaam,GEORGE FAUSTIN,kikao hicho kimemteua bwana Idrisa Washington kukaimu nafasi ya mwenyekiti Taifa na Juliana Mpanduji, kuwa kaimu katibu Mkuu,mpaka pale utaratibu mwingine wa kikatiba utakapofanyika.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts