4/22/16

Lugha nzuri yatakiwa kwa Makampuni yanayotoa huduma kwa wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro
Wadau wa utalii yakiwemo Makampuni yanayotoa huduma kwa wageni wanaopanda mlima Kilimanjaro, wametakiwa kuboresha huduma zao kwa wageni ikiwemo kutumia lugha nzuri ili kuwezesha wageni wengi kuendelea kufanya utalii wa kupanda mlima huo badala ya kuweka maslahi binafsi ya kupata fedha pekee.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki ametoa agizo hilo kwenye lango la Marangu wilayani Moshi ,wakati akifungua kampeni ya kufanya usafi wa mlima Kilimanjaro ambapo amesema serikali haitazivumilia kampuni kama hizo, kwa kuwa zinawafukuza wageni ipatia sifambaya mkoa huo

Aidha Sadiki ameitaka jamii na wadau wa maendeleo na wa utalii kushirikiana katika kampeni za kuufanyia usafi mlima huo ambao umekuwa nikivutio cha watalii duniani kote.

Mkurugenzi mkuu wa hifadhi za taifa nchini TANAPA Alan Kijazi amesema mlima Kilimanjaro ambao unasifa ya kipekee ya kusimama peke tofauti na milima mingine duniani,kuna wajibu mkubwa wa jamii kuulinda na kuktunza kwakuwa umekuwa ni kivutio chenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.

Katika zoezi la uzinduzi wa usafi wa mlima Kilimanjaro uliyoshirikisha viongozi mbalimbali wa mkoa na wilaya,na viongozi wa TANAPA na KINAPA,pamoja na wadau mbalimbali wa utalii ndani na nje ya mkoa huo,walipanda mlima huo wakiongozwa na mkuu wa mkoa Said Meck Sadik .hadi kituo cha kwanza cha Mandara kisha kurudi hadi geti la marangu.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm