4/27/16

Maamuzi mapya kwenye kesi ya aliyekuwa Kamishna mkuu wa TRA April 27 2016

April 01 2016 aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania, Shose Sinare walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kosa  la utakatishaji fedha.
Kesi hiyo imeendelea leo April 27 2016 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo Mahakama imefutilia mbali shitaka la utakatishaji fedha lililokuwa linawakabili washitakiwa wote  hivyo washitakiwa wamebaki na mashitaka saba.
Upande wa Jamhuri umekata rufaa mahakama kuu na kusababisha maamuzi ya kupewa dhamana kuahirishwa mpaka April 29 2016 ambapo mahakama itatoa maamuzi kama watuhumiwa watapewa dhamana, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts