4/23/16

Mahakama Yaamuru Nyumba Kubomolewa Segerea

 

Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imetupilia mbali kesi ya walalamikaji waliojenga maeneo hatarishi kwa maisha ya binadamu katika jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa kukosa baadhi ya majina ya walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.

Pia mahakama hiyo imetupilia kesi ya wakazi 2619 ya kupinga kubomolewa nyumba zao bila kulipwa fidia yoyote na serikali kwa wakazi zaidi ya elfu nne wa eneo hilo mara baada ya wakazi hao kukosa majina na sahihi za wananchi walioomba kuwakilishwa katika kesi hiyo.Akizungumza  jijini Dar es Salaam, Jaji Fredrica Mgaya wakati shauri hilo amesema kesi hiyo imefutwa kwa kukosa majina na sahihi za watu wanaotaka kuwakilishwa na watu wanane walioshauriana kuwa watawasimamia katika kesi hiyo ya bomoabomoa ya wakazi wa jimbo la Segerea.

Akisoma maamuzi ya wakili wa serikali Gabriel Malata amesema kuwa walalamikaji hawana kibali au viapo halali vya wakazi hao kuomba kuwakilishwa na watu walioteuliwa kuwasimamia katika kesi yao ya kubomolewa makazi yao.

Pia Jaji Fredrica Mgaya ameiomba serikali kutoa elimu kwa wakazi wa maeneo ya mabondeni ili wajue athari zitakazowakuta kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

chanzo: Mtembezi

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm