4/27/16

Masoud Kipanya Arejea Clouds FM

IMG_0659
Alipoondoka Clouds FM mwaka 2008, ilikuwa habari kubwa. Wakati huo mtandao huu nao ulikuwa mchanga lakini Masoud aliutumia kuweka mambo bayana(sio bayana sana). Akasema “Sijaacha Kazi Clouds FM”… kisha akafafanua. Mwisho wa siku Power Breakfast ikabadilika. Enzi za Masoud Kipanya na Fina Mango wakiwaamsha wasikilizaji zikafikia mwisho. Maisha yakaendelea.
Miaka takribani 9 baadae, Masoud Kipanya yupo njiani kurejea Clouds FM. Hiyo ni kwa mujibu wa Clouds FM wenyewe kupitia mitandao ya kijamii. Kurudi kwa Masoud ni furaha kwa wasikilizaji. He’s funny. He’s opinionated. Unaweza kujua upeo wake kwa kupitia cartoon zake za “Kipanya”. Ni mtu anayeitazama jamii kwa jicho la tatu.
Lakini mbali na furaha kwa wasikilizaji, kurejea kwa Kipanya “mjengoni”, ni mwendelezo wa kavita fulani la kibepari kati ya Clouds FM na Efm ambao ni wapinzani rasmi wa Bw. Kusaga na team yake. Vita ya panzi ni faida kwa kunguru. Watangazaji wanaona thamani yao. Mwisho wa siku muhimu ni content. Wanachokisema kinaeleweka? Au wametumwa?
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts