4/25/16

Matunda ya Ziara ya Magufuli Nchini Rwanda Yaanza Kuonekana

Rwanda ni nchi ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya ziara tangu awe Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa la Tanzania.
Katika ziara yake Nchini Rwanda Rais Magufuli na mwenyeji wake Paul Kagame waliweza kuzindua Daraja la Kimataifa la Rusumo, unaweza ukajiuliza ni ipi tija ya ziara ya Rais Magufuli nchini humo?

Matunda ya ziara hiyo yameanza kuonekana ambapo makundi mbalimbali ya kibiashara yakiwemo Taasisi ya kusimamia Wafanyabiashara nchini (TCCIA), Wamiliki wa Malori nchini (TATOA) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Nchini (TANTRADE), wote kwa pamoja wameandaa kongamano la kibiashara litakalofanyika Kigali nchini Rwanda ambapo wafanyabiashara zaidi ya 100 watajadili changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo mbili.

Kongamano hilo linalotaraji kufanyika mapema mwezi Mei litakuwa na tija ya kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Rwanda halikadhalika maendeleo ya kiuchumi kutokana na kuwepo kwa wafanyabiashara wengi kwa nchi hizo kufuatia uzinduzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts