Mbaroni kwa Kunywa Pombe Saa za Kazi | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

4/23/16

Mbaroni kwa Kunywa Pombe Saa za Kazi

Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais John Magufuli kwa kuwasweka rumande watu wanane waliokutwa wakinywa pombe baa wakati wa saa za kazi.


Mkuu wa Wilaya Sengerema, Zainabu Terack alitoa amri ya kukamatwa na kuwekwa mahabusu watu hao juzi baada ya kukuta baa zimefunguliwa huku wakiendelea kupata kinywaji kabla ya saa 9.30 alasiri ambao ndiyo muda wa kufunga ofisi za umma.


Serikali imepiga marufuku unywaji wa pombe, mchezo wa pool na michezo mingine wakati wa saa za kazi kama mkakati wa kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki shughuli ya uzalishaji mali katika eneo lake.


Terack aliongoza operesheni hiyo kwa dakika 45 kusaka wanywa pombe na wacheza pool muda wa kazi.


Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uzembe na kukiuka amri halali ya Serikali kwa kunywa pombe saa za kazi.


Wakijitetea baada ya kutiwa mbaroni, baadhi ya waliokutwa wakinywa pombe muda wa kazi ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai walikwenda katika baa hiyo kujiliwaza kwa msiba wa ndugu yao, Petro Shoyo na kumuomba mkuu huyo kuwasamehe kwa sababu ni kosa lao la kwanza na hawakukusudia kukiuka agizo hilo.Utetezi na ombi hilo haukufua dau mbele ya mkuu huyo baada ya kusisitiza watuhumiwa hao wawekwe mahabusu na kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho kwa wengine. 
 
Chanzo: Mwananchi

google+

linkedin