4/30/16

Mengine yalioandikwa kuhusu Jose Mourinho na Man United


Bado headlines za kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal kutimuliwa na ndani ya Man United na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho zinazidi kuchukua headlines, huu ni mtihani ambao majibu yake yatajulikana mwisho wa msimu baada ya Ligi Kumalizika.
Hadi sasa habari za Jose Mourinho kujiunga na Man United hazina uhakika wala dalili kama kweli atajiunga na Man United au la, kwani leo Sky Sports wameripoti kuwa Jose Mourinho hana makubaliano yoyote na Man United, licha ya kuwa amekuwa akiripotiwa kutaka kujiunga na Man United.
Hayo yameripotiwa na Sky Sports lakini The Sun imeandika kuwa klabu ya Man United imemuhakikishia Jose Mourinho kuichukua nafasi ya Louis van Gaal mwisho wa msimu, licha ya kuwa mwenyekiti wa Man United Ed Woodward anaripotiwa bado anafikiria juu ya maamuzi hayo ambayo yamekuwa topic kubwa katika mitandao.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts