4/23/16

Mr. Blue: Ngoma yangu na Alikiba Itakuwa Historia Kubwa

 http://biggestkaka.co.ke/wp-content/uploads/2016/02/Ali-Kiba-with-Mr.-Blue.jpg

Hitmaker wa baki na mimi ambaye hivi karibuni aliuaga ukapera kwa kuamua kufunga pingu za maisha na mzazi mwenzake Wayda, ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia kolabo yake na msanii nyota kwa sasa Alikiba aliyoipa jina la Mboga Saba.

Akizungumza na mtandao wa Mtembezi Mr. Blue amesema kuwa ngoma hiyo ipo tayari na anatarajia kuiachia wiki ijayo endapo mtayarishaji wa ngoma hiyo Man Water atamkabidhi, hivyo itakuwa rahisi kwake kuikabidhi kwa  mashabiki wake.Blue ameongeza kuwa Mboga Saba ni ngoma ya aina yake ambayo anaimani itapokelewa vizuri na mashabiki wake kwa kuacha historia ya ngoma alizowahi kuzifanya, kwani wote wawili wameonesha umahiri mkubwa, katika hatua nyingine Blue amesema mashabiki wake wajiandae pia kwa ngoma mpya ya kundi lake la B.O.B Micharazo ambayo ameirekodi kwa Man Water.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts