4/27/16

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka BRT, Watumiaji wa barabara watakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani

Wakati kipindi cha mpito cha Mabasi ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam kikiwa kinatarajiwa kuanza Mei 10 mwaka huu, uongozi wa kampuni ya UDA RT umewataka watumiaji wengine wa barabara hasa wenye vyombo vya usafiri kuzingatia sheria za barabarani wakati madereva wa mabasi hayo wakiendelea na mazoezi.

Msemaji wa Kampuni hiyo, Sabri Mabruk ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa mpaka sasa tayari mabasi ya kampuni hiyo yapatayo 4 yamechunwa na vyombo vingine vya usafiri.

Amesema miundombinu hiyo imejengwa kulingana na mahitaji, hivyo kila chombo cha usafiri kipite kwenye njia yake na hata waenda kwa miguu nao wapite katika njia yao.

Ameongeza kuwa kabla ya tarehe ya kuanza kwa usafiri huo Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) inatarajia kutangaza nauli kwa ajili ya mabasi hayo, na kuwaomba wananchi kuvuta subira kwa ajili ya suala hilo.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm