4/29/16

Mtaalamu wa Teknolojia wa Kike kaacha kazi Google na kutinga Facebook
Mwana Mama huyo Regina Duncan ambaye muda wake hapo Google umekuwa wa mafanikio makubwa anaenda kujiunga na kitengo pia cha uvumbuzi katika kampuni ya Facebook.
Regina Duncan

Mfano miradi ya kutengeneza tatoo ya kidigitali na pia miradi miwili iliyo kuwa inatengeneza simu janja ilimjengea sifa kubwa katika kampuni hiyo ambapo ilitokana na ubunifu wake.

Facebook wamempata mtu muhimu hasa katika kipindi ambacho mtandao huu unayo miradi mingi ambayo inayohitaji kiongozi ambaye ana jicho na mtazamo wa ki bunifu kama Regina Duncan. Makampuni makubwa sio jambo geni kwa kuajiri wafanyakazi ambao walikuwa katika kampuni ambayo ni mpinzani wako ila ni ukweli usiofichika kwamba Google imempoteza mtu ambaye alikuwa na mafanikio katika kazi alizofanya.

Mama huyo kapewa kitengo Facebook ambacho kinaitwa Building 8 na alipo ulizwa kuhusu kuhama Google amesema kwamba hii ni nafasi yake kufanya kile kitu alikuwa anatamani kufanya siku nyingi na anahuzunika saana kuondoka Google.Lakini Google wanasema kwamba wanamtakia kila la kheri mfanyakazi wao huyo wa zamani katika majukumu yake mapya ambayo ni Facebook.
Na Clement Silla Chanzo:Theverge.com
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm