4/24/16

Ofisa elimu Iringa aungana na walimu kufundisha


Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wa Manispaa ya

Iringa. Ofisa Elimu wa Shule za Msingi wa Manispaa ya Iringa, Haji Mnasi  ameungana na  walimu wake kuingia darasani na kufundisha ikiwa  ni utekelezaji wa mataala kwa vitendo.
Mnasi amefikia uamuzi hi kwa kilie alichodai ni kutekeleza kwa vitendo kauliya hapakazi tu akiwa na dhamira ya kuwatia morali walimu ya kufundisha kwa bidii na kuwezesha halmashauri hiyo kufikia lengo iliyojiwekea kufaulisha kwa asilimia 98 katika msimu wa ujao.
“Matokeo  ya mwaka jana Manispaa tulifikia asilimia 85.5 na sasa tumeweka lengo la kufikia asimilia 98 lengo langu la kufanya ziara na kuingia darasani kufundisha ni kusaidia kuamusha morari ya walimu ya kufundisha,hii inatokana na walimu wengi kukata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali ambazo kwa sasa serikali inazishughulikia”alisema Mnasi.
Mnasi alisema kuanzaia sasa atafanya ziara nyingi mashuleni ili kujionea utendaji kazi lakini pia katika ziara hizo amewaagiza waratibu elimu kata kumuandalia vipindi ili aweze kuingia darasani na kufundisha.
Akizungumza changamoto zinazowakabili walimu katika Manispaa hiyo alisema ni upandishaji wa madaraja na upatikanaji wa sitahiki zao ambapo alisema kwa sasa changamoto zote zimefanyia kazi na zimefikia hatua nzuri na kwamba mda simrefu kilio cha walimu juu ya stahiki zao kitabaki historia.
“Suala la madaraja tumeshalishughulikia jambo lililobaki ni lile la stahiki zao na tumeshalifikisha ngazi za juu linafanyiwa kazi ninaimani kuwa jambo hilo linakwenda vizuri na mda simrefu litabaki historia,”alisema Mnasi.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts