4/26/16

Rais Magufuli Atoa Msamaha kwa Wafungwa 3,551

 
Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wafungwa 580 wataachiwa huru huku 2,971 waliosalia watapunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.
Miongoni mwa wafungwa watakaonufaika na msamaha huo ni wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 70, wenye ulemavu wa akili na wale waliothibika kuwa na ugonjwa wa Ukimwi na saratani.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts