4/23/16

SHERIA INAYOMPA MAMLAKA RAIS MAGUFULI KUMUACHIA HURU BABU SEYA

‘Babu Seya’ na ‘Papii Kocha’ walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji na kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa,   Sinza   Dar es Salaam.

Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto hao wa shule ya msingi waliokuwa na umri kati ya miaka sita na minane.

Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo kati ya Aprili na Oktoba 2003.

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliwatia hatiani Babu Seya na wanae kwa   hatia ya kubaka na kulawiti.

Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi yao.

Hukumu hiyo ilitolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliyewatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25, 2004.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari 2010.

Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia huru watoto wake wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza.

KIPI KINACHO ENDELEA?

Machi 11, Mwaka huu Rufani ya kesi yake ilitua kwenye Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) na haikusikilizwa kwenye mahakama ya wazi.

Sasa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Rais aliyopo madarakani ndiye mwenye mamlaka pekee ya kumuachia huru.

katiba
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts