4/23/16

Shule Zafungwa Baada ya Choo Kutitia

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi,
Moshi.  Wanafunzi wa shule za msingi za Kimanganuni na Mawela zilizopo Kata ya Uru Kusini wilayani Moshi wamepewa likizo ya siku kumi baada ya choo cha shule hizo mbili kutitia ardhini kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo, mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Flugence Mponji amesema kutitia kwa choo hicho kumesababisha wanafunzi kukosa sehemu ya kujisaidia.
Mponji amesema kutokana na tatizo hilo imewalazimu kuwapa likizo ya wiki mbili wanafunzi wa shule hizo pamoja na walimu wao ili kukijenga.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm