4/29/16

Tanzanite Amuomba Radhi Diamond Platnumz


Raha ya msamaha mwenye kuombwa msamaha aitikie kwa kukubali msamaha,unakumbuka wimbo wa pili wa Diamond Platnumz uliompa dili nyingi unaoitwa Mbagala aliofanya kwa Bob Junior?
Msanii Tanzanite kwa sasa amebadili jina na kujiita Tanzamagic akisimamiwa na legendari wa Bongo Fleva hapa nchini Prince Dully Sykies amewaangukia na kuomba radhi mashabiki wake wa muziki huo.
“Habari ndugu zangu naomba radhi, yawezekana ikawa utoto lakini ilikuwa katika mipango ya kutafuta riziki. Wimbo wa Mbagala niliubadilisha na kuitwa uchawi na wanga nikawagawa mashabiki na kufanya waamini ni wimbo wangu; naomba radhi” amesema Tanzanite kupitia XXL ya Clouds Fm.
Diamond bado hajajibu kama amemsamehe Tanzamagic ama la ! huku Dully Sykes akisisitiza kutotoa ngoma za msanii huyo hadi pale Chibu Dangote atakaporidhia msamaha huo.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts