4/22/16

Tetesi za Ali Kiba Kuacha Muziki....Ukweli Huu Hapa

“Mimi ni Muislamu na ninajivunia kuwa hivyo nahisi ninakoelekea ni kubaya zaidi ni kheri nijivue mapema nitubie kwa niliyoyafanya” maelezo hayo ni kwamujibu wa ukurasa mmoja wa facebook unaoitwa @Tanzania Yetu

.IMG_20160422_141029_776

Mtandao Huu umemtafuta Kibabude ambaye ni Meneja wa Ali Kiba kuhusu ‘issue’ hiyo ambapo amebainisha kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na kwamba Ali Kiba hajawahi kufikiria kustaafu muziki na kuwataka mashabiki wapuuze maneno hayo.

“Ali hajafikiria wala kuwaza kuacha muziki kwa sababu kuna vitu vingi vya kufanya hatujawatendea haki wapenzi wetu hayo ni maneno ya watu”.

Meneja huyo ameweka wazi kuwa matarajio ya Kiba kwa sasa ni kuachia ngoma mpya ya Aje mwezi ujao ambayo amefanya mwenyewe na itaambana na video aliyoifanya Bongo na South Africa.

chanzo: Mtembezi

Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm