4/29/16

Tizeba alia na jipu Buchosa
Mbunge wa Buchosa, Dk Charles Tizeba amesema mradi wa maji wenye thamani ya Sh1.6 bilioni unaoratibiwa na Wizara ya Maji kuanzia Lumeya hadi Nyehunge katika halmashauri hiyo, umekwama kukamilika tangu ulipoanza mwaka 2012.


Dk Tizeba amesema mradi huo unaojengwa na Kampuni ya Pet Cooperation haujakamilika, huku wananchi wakihangaishwa na uhaba wa maji.


Amesema kulingana na mkataba, mkandarasi alipewa kazi ya kutekeleza mradi huo tangu 2012 na alipaswa kuukamilisha ndani ya miezi sita, lakini hadi sasa haujakamilika wakati wananchi wanazidi kuteseka.


“Inanisikitika kuona kampuni iliyopewa mradi huu kutokamilisha kwa wakati huku Serikali ilishatoa fedha, mabomba yenyewe yametandazwa yako nje na mkandarasi huyu bado hajachukuliwa hatua,” amelalamika Dk Tizeba.


Mhandisi wa Maji wa halmashauri za Sengerema na Buchosa, Nicas Ligombi amesema sababu zinazofanya kampuni kutokamilisha miradi kwa wakati ni tamaa ya kuwa na zabuni nyingi wakati uwezo wa kumudu ni mdogo.


“Mradi huo wa Lumeya hadi Nyehunge uliolenga kuwahudumia wananchi 1,600 tayari mkandarasi alishachukua Sh1.3 bilioni kati ya Sh1.6 bilioni,” amesema.
 
mwananchi
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts