4/27/16

Uko Wapi Uhuru wa Vyombo vya Habari

 

Januari 26 mwaka huu serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ilitangaza kusitisha rasmi urushaji wa moja kwa moja wa matangazo ya Bunge, sababu kuu ikitajwa kuwa ni ufinyu wa bajeti.

Hivi sasa wananchi hawalioni tena bunge moja kwa moja likiendelea na mijadala yake kama ilivyozoeleka na badala yake wanasubiri hadi linakiliwe ndipo waone kile ambacho serikali inataka!

Suala hili linanisukuma kuiuliza serikali iliyopo madarakani kuwa, uko wapi uhuru wa Vyombo vya Habari hapa nchini kwani vyombo binafsi pia vimezuiwa kuonesha matangazo hayo moja kwa moja licha ya kuwa na uwezo wa kumudu gharama za urushaji matangazo.

Tunapoelekea katika Maadhimisho ya siku ya Vyombo vya Habari Duniani ambayo huadhimishwa Mei 2 na 3, kila mwaka huku yakipangwa kufanyika nchini Finland mwaka huu, serikali itazame upya suala la urushaji matangazo ya bunge nchini Tanzania kwani inawanyima wananchi wake haki ya msingi  ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati.

Uzuiaji wa urushaji matangazo ya moja kwa moja katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unalenga kufifisha uhuru wa Vyombo vya Habari licha ya kuwa na idadi kubwa ya vituo vya redio, televisheni na magazeti.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts