4/26/16

Vurugu za Kisiasa Burundi, ICC kufanya uchunguzi wa uhalifu wa kivita.


Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC iliokpo mjini The Hague, imesema itafanya uchunguzi juu ya madai ya kukamatwa watu hovyo na kuwekwa ndani pamoja na machafuko nchini Burundi, mambo ambayo yamekuwa yakiripotiwa tokea kuzuka kwa mgogoro wa kisiasa mwaka mmoja uliopita.

Ofisi ya kamishna wa haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa inakadiria kwamba watu 430 wameuawa tokea mwezi Aprili mwaka uliopita, wakati Rais Pierre Nkurunziza alipoanza mkatati wa kugombea muhula watatu na baadae kushinda uchaguzi mwezi Julai uliosusiwa na vyama vya upinzani ambavyo vimeshikilia kwamba muhula wa tatu ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICC Fatou Bensouda alitangaza kuanza kwa uchunguzi wa awali akisema ameziona ripoti za watu kuwekwa magerezani , mateso na ubakaji. Katika taarifa yake Bensouda alisema kiasi ya watu 3,400 wamekamatwa.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts