4/26/16

Wacheza ‘vigodoro’ Kimanga waonywa


WANANCHI wa kata ya Kimanga, jijini Dar es Salaam, wameonywa juu ya tabia ya kuweka ngoma za usiku maarufu kigodoro kwenye makazi na badala yake wametakiwa kufanyia kwenye kumbi za sherehe.
Akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kimanga, eneo la ABC juzi, wakati wa uzinduzi wa kikundi cha polisi jamii, Diwani wa kata hiyo, Manase Mjema, alisema ngoma hiyo mbali na kuwa kero, pia imekuwa ikisababisha watu kuibiwa na kuporwa mali zao kutokana na vijana wahuni kujiiingiza na kuvizia maeneo yaliyo karibu na ngoma hizo.
“Inasikitisha sana kuona kuna watu bado wanatoa vibali vya ngoma hizi, hatutakubali watu wanaibiwa na kuporwa hivyo katika kata hii kama mtu atakuwa na ngoma mwisho saa 12:00 jioni ikiwa zaidi ya hapo wafanyiwe ukumbini ili wahudhurie walioalikwa,” alisema.
Mjema alisema siku za karibuni kumekuwa na matukio mengi ya watu kukatwa mapanga na kuporwa mali zao katika kata hiyo kutokana na ngoma hizo ambazo zimeshapigwa marufuku na kuonya kuwa kama akitokea mkazi wa maeneo hayo ataweka ngoma hiyo, atakamatwa na vifaa vyote vilivyotumika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Nae Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata, Mrakibu Msaidizi, Bakari Goti, alisema hali hiyo haitavumilika si kwa Kimanga pekee, bali Tabata nzima, kwani vitendo vya kihalifu vimekithiri na kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoathirika.
“Kwa kuwa sheria zipo na zinaeleweka basi kwa usiku wahusika wakodi ukumbi ili vijana hao wahalifu wasipate nafasi ya kudhuru watu na mali zao, vinginevyo atakayehusika hata kama hatukumkamata usiku ule, tukisikia tu tutamtafuta kesho yake na kumchukulia hatua,” alisema.
Awapongeza wananchi wa Kimanga kwa kuanzisha ulinzi shirikishi na kuwasihi kuharakisha michango ambayo itagharamia walinzi walioandaliwa kwa ajili hiyo.
Alisema mbali na kulinda usiku, pia kuna haja ya kuwapo kwa doria za mchana kwani kumeanza kuripotiwa matukio ya watu kuvamia nyumba na kuiba mchana na aliwashauri wananchi kujenga tabia ya kuwatambua majirani na kubadilishana namba za simu ili iwapo kutatokea tukio la uhalifu katika moja ya nyumba iwe rahisi kupeana
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts