4/25/16

Wakenya Watinga Kaburini Kwa Kanumba, Wamuenzi!


KANUMBA
Mwigizaji wa Kenya, Juma Shibe ‘MJ’ (kulia), meneja wake Khalifan Ally wakiwa na mama Kanumba kwenye kaburi la mwanaye.

DAR ES SALAAM: Tutakukumbuka daima! Mwigizaji wa Kenya, Juma Shibe ‘MJ’ akiambatana na meneja wake, Khalifan Ally, wametinga kaburini kwa aliyekuwa staa wa Bongo Muvi, Steven Kanumba kwenye Makaburi ya Kinondoni, Dar kwa lengo la kumuenzi jamaa huyo na kumfariji mama yake, Flora Mtegoa ikiwa ni miaka minne tangu kifo cha mwanaye.
Kanumba-612Marehemu Kanumba
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Wikienda lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo jamaa hao waliambatana na mama Kanumba ambaye kama kawaida yake alikuwa akiangua kilio muda wote.
Wakiwa kaburini hapo, waliweka mashada na kumuombea marehemu ndipo mama huyo akatokwa na machozi kwa kuona vijana hao wamefunga safari kuja Bongo kwa ajili ya Kanumba.
Kwa upande wake MJ alisema: “Kanumba alikuwa mtu muhimu, alinishawishi kuingia kwenye sanaa, siku chache kabla ya kifo ilikuwa tucheze filamu ya pamoja.”

GPL
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm