4/29/16

Wanaume Watakiwa Kwenda Kliniki
Mkuu wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Joshua Mirumbe amewataka wanaume kujengea tabia ya kuwapeleka watoto wao kliniki ili nao wapate elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.


“Jukumu la kuangamiza malaria ni letu sote, hivyo hata wanaume hatuna budi kushiriki kupeleka watoto kliniki maana huko kunatolewa elimu ya jinsi ya kujikinga,” amesema Mirumbe.


Mirumbe amesema wanaume wakihudhuria kliniki kama wanavyofanya wanawake, watapatiwa elimu mbalimbali za afya ya jamii.


Mratibu wa Ugonjwa wa Malaria wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Dk Raymond Mzungu amesema maambukizi katika halmashauri hiyo yamepungua kutoka asilimia 38 mwaka 2010 hadi 21, mwaka jana.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts