Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

4/27/16

Waziri Simbachawene aifuta Bodi ya Machinga Complex

Waziri Simbachawene aifuta Bodi ya Machinga Complex
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene ameifuta Bodi ya usimamizi wajengo la Machinga Complex la jijini Dar es Salaam na kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alisimamie kwa kuhakikisha kuwa linatumiwa na wafanyabiashara wadogo wasiokuwa na maeneo maalumu ya kufanyia biashara.
Mhe Simbachawene ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya yaWafanyabishara Tanzania (JWT) leo jijini Dar es Salaam ambapo miongoni mwa changamoto ambazo wafanyabiashara hao wamezieleza ni pamoja na kukosekana kwa uwazi wa ulipaji kodi upande wa bandarini, ukosefu wa maeneo maalum ya kufanyia biashara na uwepo wa usumbufu wa upatikanaji wa leseni za biashara.
"Naomba Mkuu wa mkoa usimamie jingo hili kwa kuhakikisha wale wafanyabiashara wadogo wadogo waliopo pembezoni mwa barabara maeneo ya karume na wengine wasio na sehemu za kufanyia kazi kufanya biashara zao hapo" alisema Mhe.Simbachawene
Amesema wafanyabishara ndogo ndogo wanatakiwa kunufaika kwa kupatiwa maeneo maalum ya kufanyia kazi huku akieleza kuwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha inatenga maeneo hayo likiwemo jengo la Machinga Complex ambalo lilijengwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo.
Aidha, Mhe. Simbachawene amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa walezi wa Jumuiya za Wafanyabiashara katika mikoa na wilaya zao ili kupata nafasi ya kukaa nao pamoja na kujadili matatizo mbalimbali yanayowakabili na namna ya kuyatatua.
Pia ameagiza Wakurugenzi wa Halmashauri kuweka utaratibu maalum wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara zaidi ya mara mbili kwa mwaka ili kupata nafasi ya kujadiliana nakuangalia matatizo yanayowakabili wafanyabiashara na kwa pamoja kutafuta suluhisho la matatizo hayo.
Mhe.Simbachawene amezitaka Halmashauri kutokutumia nguvu katika kukusanya kodi na amezitaka zishirikiane na wafanyabiashara kwa kuwapatia elimu ya umuhimu waulipaji kodi ilikuwepo na uwazi na uwajibikaji kati ya pande zote mbili.
"Naomba tuondokane na dhana ya mgambo kunyang�anya wafanyabiashara bidhaa zao na badala yake uwekwe utaratibu wa kuwapatia elimu ya mlipa kodi ili waweze kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyari kwa maendeleo yaTaifa," alisema Mhe.Simbachawene.
Waziri Simbachawene pia ameahidi kusimamia uwazi na uwajibikaji katika ulipaji kodi kwa kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za ulipaji kodi zinafuatwa ili kuondokana na upatikanaji wa mianya ya rushwa kwa watendaji wa serikali na wafanyabiashara wasio waaminifu wanaoliletea Taifa hasara.
Katika mkutano huo, Mhe. Simbachawene ameahidi kuyasimamia mapendekezo yaliyotolewa na Jumuiya yaWafanyabiashara Tanzania likiwemo suala la kuwepo kwa uwazi katika ulipaji wa kodi bandarini, kuboresha taratibu za utoaji leseni ambapo wafanyabiashara hao wamependekeza leseni ziwe zinatolewa kwa kipindi cha miaka mitano au mitatu na kulipia ada tu kila mwaka badala ya utaratibu wa sasa unaowataka kulipia leseni kila mwaka pamoja na kuwepo kwa udhibiti wa utoaji holela wa leseni za biashara kwa wafanyabiashara wageni.
Aidha, Mhe. Simbachawene aliziagiza halmashauri kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/17 kuacha kuwatumia Mawakala katika kukusanya mapato na kuhakikisha malipo yote yanayofanywa yafanyike katika akaunti za halmashauri badala ya Mawakala binafsi.
"Kwa vile vyanzo vigumu sana vya kukusanya mapato, halmashauri zilete maombi hayo maombi hayo wizarani na kuyafanyia tathmini kabla ya kutumia wakala," alisisitiza Mhe. Simbachawene.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Johnson Minja aliiomba Serikali kuboresha mazingira ya wafanya biashara ili kuwa na walipa kodi halali watakao kuza uchumi wa nchi kutoka uchumi wakati hadi uchumi wa viwanda na hivyo kukuza pato la taifa.