Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/2/16

75,000 Waanza Mtihani Kidato cha Sita

WAT A H I N I WA 74,920 leo wanaanza kufanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Sita katika shule mbalimbali nchini huku watahiniwa 11,597 wakifanya mtihani wa Ualimu.
Ofisa Habari wa Baraza la Mitihani (NECTA), John Nchimbi aliliambia gazeti hili kuwa mtihani wa kidato cha sita unaanza leo hadi Mei 19, mwaka huu. Nchimbi alisema kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 65,610 ni watahiniwa wa Shule huku watahiniwa wa Kujitegemea wakiwa 9,310.
“Kati ya watahiniwa wa shule 65, 610, watahiniwa wasichana ni 24,549 na wavulana ni 41,061 huku watahiniwa wa kujitegemea wasichana wakiwa ni 3,176 na wavulana ni 6,134,” alisema Nchimbi.
Kwa upande wa mtihani wa ualimu, Nchimbi alisema kati ya watahiniwa 11,597 watakaofanya, watahiniwa 10,942 wanafanya Ualimu Daraja A na watahiniwa 654 wanafanya mtihani wa Stashahada ya Sekondari na mmoja anafanya Stashahada ya Ufundi.
“NECTA inatoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa, na wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu. “Kwa wanafunzi tunaamini walimu wamewaandaa vizuri, na ni matarajio yetu wanafunzi watafanya mitihani yao kwa kuzingatia taratibu zote za mitihani ili matokeo ya mitihani yaoneshe uwezo wao halisi kulingana na maarifa na ujuzi waliopata katika kipindi walipokuwa shule,” aliongeza Nchimbi.
Aidha, Nchimbi alitoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa kuhakikisha mtihani unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza kuwa mtu asiyehusika na mtihani asiingie kwenye eneo la mtihani.