5/1/16

Al Shabab waua wanajeshi 30 wa SomaliaWapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, Al Shabab wanasema wamewauwa wanajeshi wa serikali zaidi ya 30.

Al Shabab, wanadai kutekeleza mauaji hayo walipoteka tena kijiji cha Runorgood, Kaskazini-Mashariki mwa mji mkuu wa Somali Mogadishu.

Wenyeji wa kijiji hicho wamethibitishia BBC, kwamba kijiji chao kinadhibitiwa tena na wanamgambo wa Al Shabab.

Wapiganaji hao walikuwa wametimuliwa kutoka kijiji hicho hapo jana.

Kwengineko nchini Somalia, watu kama watatu waliuwawa, kwenye shambulio la bomu, katika soko la mifugo huko Qoryoolay, inavoelekea shambulizi hilo lililengwa maafisa wa kukusanya kodi wa serikali.-BBC
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm