Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/20/16

Arusha Yaingia Tena Kwenye List ya Makosa ya Mtandao

 

Siku chache baada ya Kituo cha Sheria na Msaada wa Haki za Binadamu (LHRC) kuhimiza na kutoa rai kwa Watanzania kufanya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, mwitikio bado umekuwa mdogo baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Arusha kumshikilia Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange.

Kijana huyo kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook alisambaza ujumbe wenye maneno makali juu ya viongozi hao na kutoa taarifa za uchochezi akimtaka Mkuu wa Majeshi kupindua nchi kutokana na viongozi wote wa juu kuwa nje ya nchi huku kukisalia pasipo kiongozi wa kukaimu nafasi hiyo.

“Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti” hayo ni maneno yake mtuhumiwa yaliyonukuliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo na kuongeza kuwa mtuhumiwa alitoa maneno makali pia kwa Dk. Shein kwa kusema “Dk. Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba Mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”.

Mkumbo amesema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika, huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia pasipo kukiuka sheria na taratibu za kisheria .

Hili sio kosa la kwanza kuripotiwa juu ya matumizi mabaya ya Mitandao ya Kijamii kwani Isaac Abakuk (40) mkazi wa Olasiti jijini Arusha pia alipandishwa kizimbani Mahakama Kuu Kanda ya Arusha baada ya kumtukana Rais Dk. Magufuli katika ukurasa wake wa Facebook ambapo ushahidi umekamilika na kesi yake itaanza kusiklizwa mfululizo kuanzia June 5 mwaka huu.