5/16/16

Auawa kwa Kukatwakatwa na Kisu kwa Wivu wa Kimapenzi

MKAZI wa kitongoji cha Ukolo, kijiji cha Chala B wilayani Nkasi, Moses Nambasita (48), ameuawa kwa kuchomwa visu mwili mzima kutokana na wivu wa kimapenzi.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Vincent Mwanambuu, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni, baada ya Nambasita kuvamiwa na Peter Kiberenge (45) alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda nyumba ya jirani.

Alisema baada ya kupata habari hiyo, alitoa taarifa katika kituo kidogo cha polisi Chala na walifika na kuichukua maiti kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi na kuanza kuwasaka watuhumiwa.

Kwa mujibu wa Mwanambuu, tukio hilo lilitokana taarifa alizopewa mtuhumiwa na ndugu zake kuwa Nambasita alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake, ambaye waliachana muda mrefu.

Alidai kuwa kutokana na taarifa hizo, mtuhumiwa alipeleka shauri hilo la ugoni katika Mahakama ya Mwanzo Chala na sasa wanashangaa kuona ameamua kujichukulia sheria mikononi na kuwa baada ya kutekeleza unyama huo, alikimbia na kwenda kusikojulikana.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Godfrey Mwanakatwe, alisema kutokana na mazingira hayo, jeshi la polisi liliamua kuwashikilia watu wanne kwa tuhuma za kushiriki katika mauaji hayo, baada ya kutoa taarifa kwa muuaji kuwa marehemu ana uhusiano wa kimapenzi na mkewe huyo wa zamani.

Wanaoshikiliwa na polisi Mzee Eusebius (66), Revocatus Kiberenge (23), Giles Kiberebge (36).
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts