5/21/16

Bajeti ya Kwanza ya Serikali ya Magufuli Kusomwa Juni 8, 2016

 

BAJETI ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli itasomwa Juni 8 mwaka huu badala ya Juni 9  katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.

Akisoma matangazo mbalimbali bungeni jana, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga

, alisema uamuzi huo ulifikiwa na Kamati ya uongozi ambayo ilikutana juzi na kusema Juni 8 mwaka huu ndio siku ambayo nchi nyingine za Afrika Mashariki zitasoma bajeti zake.

“Baada ya kikao cha Kamati ya uongozi imeamuliwa kuwa bajeti ya serikali itasomwa Juni 8 mwaka huu badala ya Juni 9 kama ilivyotangazwa awali, siku ambayo nchi nyingine za Afrika Mashariki zitasoma bajeti zao,” alisema Giga.

Hata hivyo, tarehe ya kuahirishwa kwa bunge itabaki kuwa ileile ya Julai Mosi mwaka huu huku Dk. Mpango akitazamiwa kuwasilisha Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano kuanzia 2015/16 hadi 2020/21.

Awali katika taarifa ya bunge ilisema bajeti hiyo itawasilishwa rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango saa 10 kamili jioni siku ya Jumatano baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi asubuhi siku hiyo.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts