Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/6/16

Barabara za mchepuko Dodoma zitajengwa miaka 100 ijayoWIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema ina mpango kabambe wa kujenga barabara za mchepuko katika Manispaa ya Dodoma na nje ya hapo katika kipindi cha miaka 100 ijayo.

Akizungumza bungeni Dodoma jana, Naibu Waziri, Edwin Ngonyani alisema utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo utaanza rasmi pindi fedha zitakapopatikana.

Ngonyani alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM) aliyetaka kujua hatua zilizoanza kuchukuliwa hadi sasa na Serikali kutokana na ahadi aliyoitoa Rais John Magufuli wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi ya kujenga barabara za mchepuko katika manispaa hiyo.

Aidha, Bura alitaka kufahamu ni lini ujenzi wa barabara maarufu ya Great North ambayo hadi sasa ni sehemu ya Tanzania pekee ndio haijakamilika, itakamilika lini.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri huyo alimtaka mbunge huyo asiwe na wasiwasi kwa kuwa aliyetoa ahadi ya ujenzi wa barabara hizo za mchepuko wakati akiwa Waziri wa Ujenzi ndiye Rais wa Tanzania.

“Labda nikujulishe tu hapa nina ramani, tayari kuna mpango kabambe wa kujenga barabara za mchepuko ndani na nje ya manispaa ya Dodoma katika kipindi cha miaka 100 ijayo,” alisisitiza.

Alisema katika mpango huo kwa mji wa Dodoma kutakuwa na barabara nane za mchepuko zenye urefu wa kilometa 147.

Akijibu swali la Barabara ya Great North, Waziri huyo alisema kipande cha barabara yenye urefu wa kilometa 8.65 eneo la Msalato ni sehemu ya barabara ya Dodoma-Kondoa-Babati yenye urefu wa kilometa 251. Alisema barabara hiyo inaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na imegawanyika katika sehemu tatu.