5/17/16

Bunge Linatunyima Uhuru wa Kuongea Ukweli-Zitto

 

Akichangia Hotuba ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Zitto amesema siku walipochangia kauli ya serikali kuhusu bunge kutorushwa live wabunge waliokataa kuunga mkono serikali wameitwa kuhojiwa.

”Mimi nashangaa sana siku Waziri Nape ametoa kauli ya serikali kuhusu kurushwa kwa matangazo ya Bunge wabunge tulichangia wapo waliounga mkono na wengine tukakataa kuunga mkono” Amesema Zitto.

”Mheshimiwa Naibu Spika kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Waziri Nape kwenye Kamati ya Maadili mimi jana nimepata barua kwamba mnatubana kusema mnazuia bunge lisionekane hata kutoa maoni ndani ya bunge mnatuita kwenda kuhojiwa, mnaturudisha nyuma namna hii? Amehoji Zitto.

Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts