Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/5/16

CCM Kilombero Watimuana


Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Kilombero imemsimamisha kazi katibu wa siasa na uenezi wilaya Pelegrin Kifyoga kwa madai ya kwenda kinyume na maadili ya chama hicho hususani wakati wa uchaguzi mkuu 2015. Sambamba na kiongozi huyo wa juu pia halmashauri hiyo imewaondoa madarakani wenyeviti 7 wa kata na kumvua uanachama mwenyekiti mmoja wa kata kwa sababu mbalimbali.
Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu kutoka wilayani humo, katibu wa ccm wilaya ya Kilombero Bakari Mfaume amesema kwa sasa hayuko tayari kutaja sababu ya kuwasimamisha na kuwavua nyadhifa zao viongozi hao lakini imeelezwa kuwa ni kukisaliti chama hasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Mfaume amesema Kifyoga amesimamishwa nafasi yake ya uongozi na suala lake linaendelea kushughulikiwa huku viongozi waliotimuliwa nafasi zao zitajazwa katika uchaguzi wa chama utakaofanyika wakati wowote baadae.
Wenyeviti waliotimuliwa ambao hakupenda kutaja majina yao ni wa kata za Ifakara,Viwanja sitini,Signal,Mchombe,Mlimba,Mbasa na Kibaoni.
Mwenyekiti aliyevuliwa uanachama ni wa kata ya Mofu huku pia makatibu wa kata za Ifakara,Mlimba na makatibu wenezi wa kata za Kibaoni na Mofu pia wamevuliwa nyadhifa zao.
Mfaume amesema kikao hicho cha halmashauri kuu ya ccm wilaya kilikutana April 26 mwaka huu chini ya mwenyekiti wake Abdallah Kambangwa kiliridhia hatua hizo za kinidhamu zilizochukuliwa kwa viongozi hao na kuagiza hatua hizo ziendelee kuchukuliwa kwa kuzingatia haki,maadili na bila kumuonea mtu.
Amesema katika kikao hicho pia walijadili uhai wa chama,maagizo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli, aliyoyatoa katika kikao alichofanya na wenyeviti na makatibu wa mikoa na wilaya,ziara ya mwenyekiti wa ccm wilaya na tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Halmashauri hiyo ya chama imepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata haki anayostahili,kuufaidi utanzania wake na kupambana na rushwa na ufisadi kila kona ya nchi. Aidha halmashauri imeagiza chama katika ngazi zote kufanya sensa ya wanachama na mabalozi kwa lengo la kuwatambua na kuwashirikisha katika kazi zote zinazohusu uhai wa chama .
Wilaya ya Kilombero ina halmashauri mbili za Mlimba na Kilombero pamoja na mji mdogo wa wilaya hiyo, zinaongozwa na wabunge wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.