Contact us: yuvinusm45@gmail.com | email: yuvinusm45@gmail.com

We're Coming Soon

Tutarudi Baada ya Matengenezo

Tupo kwenye matengenezo ya Mtandao Wetu Tutarudi Mchakato Ukishakamilika, Tunaomba Radhi kwa Usumbufu Utakaojitokeza!

We are working very hard on the new version of our site. It will bring a lot of new features. Stay tuned!


days

hours

minutes

seconds

Subscribe to our newsletter

Sign up now to our newsletter and you'll be one of the first to know when the site is ready:

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger
Design by Yuvinusm

5/24/16

Chuo cha CBE wameyazungumza haya baada ya kuripotiwa kwa tuhuma za ufisadi chuoni hapo

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kimewataka wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari Hapa nchini kuhusu chuo hicho.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa chuo hicho Prof. Emmanuel Mjema amesema tuhuma za kuwa chuo hicho kina ubadhirifu wa kutisha si za kweli na zinalenga kuchafua taswira ya chuo hicho…..

>>>“Chuo kinafanyiwa ukaguzi wa Hesabu zake na Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali na kwa kipindi cha miaka minne tumepata hati safi (clean audit report) kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2014/2015 .” :- Prof. Mjema.

Prof. Mjema amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikijiendesha bila kupata ruzuku toka Serikalini na pia kuzalisha mapato ya ziada zaidi ya bilioni moja kwa kwa kila mwaka wa fedha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Ameongeza kuwa kutokana na Mafanikio hayo chuo hicho kimeweza kuanzisha Kampasi ya Mbeya ambapo chuo hicho kimenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 54.9 na pia maboresho katika maktaba ya chuo yamefanyika. Mafanikio mengine ni kujenga hema kubwa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 740 na kuboresha karakana ya vipimo na mizani chuoni hapo.


#MillardAyoUPDATES Mkuu wa Chuo cha CBE, Prof Emmanuel Mjema amekanusha taarifa zilizotolewa na magazeti mawili (Dira na Sema Usikike) yaliyoeleza kuwa kuna ufisadi wa kutisha Chuo cha CBE, Mjema amesema taarifa hizo si za kweli na hakuna ubadhirifu wowote katika Chuo hicho kwani wamepata hati safi kwa wakaguzi CAG, PPRA. Chuo kimepanga kumshitaki mwandishi huyo na kinamtaka akanushe taarifa hiyo.