5/24/16

CUF wapinga kuzimwa simu feki

JUMUIYA ya Vijana wa Chama cha Wananchi (Juvicuf), imepinga hatua ya serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuzima simu bandia kwa madai kuwa mpango huo umetawaliwa na ubabe na rushwa.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Juvicuf, Hamidu Bobali, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati wa uzimaji simu. TCRA inatarajia kuzima simu hizo Juni 16, mwaka huu.

Alisema serikali haitekelezi azimio hilo kwa lengo la kuwasaidia wananchi bali kuwaumiza.

Alisema pia kumekuwapo na uagizaji holela wa simu katika soko nchini na baadhi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya chini ili kuvutia wanunuzi.

Alisema bidhaa hizo zimekuwa zikiuzwa madukani na wanunuzi kupatiwa risiti za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zinazoashiria kuwa ni biashara halali kati ya muuzaji na mnunuzi.

“Juvicuf inaitaka serikali hususani Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), kufanya uchunguzi wa kina unaoweza kutuwezesha kubaini harufu ya rushwa katika kipindi hiki kuelekea kuzimwa kwa simu hizo zinazoitwa feki,” alisema. 
 
chanzo: Nipashe
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm