5/1/16

‘Freedom’ si wimbo wa siasa – Sugu


Ng’ombe hazeeki maini. Hilo amelithibitisha mkongwe wa Hip Hop Bongo, Sugu kwenye wimbo wa ‘Freedom’.
Sugu
Kutokana na kuwa chama pinzani kwenye siasa, mashabiki wengi wanafikiria kuwa jina la nyimbo hiyo ‘Freedom’ imelenga kwenye upande huo wa siasa.
Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Sugu amekanusha Freedom kuwa wimbo wa siasa.
“Hapana Freedom ni nyingine, Freedom ni mtu kuweza kuwa huru kuweza kurudi tena studio. Master J, MJ, Daxo Chali kufanya kile nachopenda kufanya na kuweza kufanya kile ambacho kule nyuma nilishindwa kukifanya. Kwahiyo sasa hivi ninaweza kusema nina Freedom. Freedom inabeba mambo mengi ikiwemo kukataa kuwa kwenye stress,” aliongezea.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts