Hatima ya madaktari, wauguzi Mei 15 | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/3/16

Hatima ya madaktari, wauguzi Mei 15
Hatima ya madaktari watano na wauguzi watano wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Butimba na ile ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou-Toure waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za uzembe uliosababisha vifo vya watoto watatu, itajulikana kabla ya Mei 15.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema leo kuwa, ofisi yake tayari imepokea na inapitia ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa kuchunguza matukio hayo mawili.


“Naendelea kuipitia kwa makini taarifa ya kamati hiyo kujiridhisha na yaliyomo pamoja na uchunguzi wa vyombo vya dola; hili ni jambo nyeti linalohitaji umakini mkubwa kuepuka madhara yanayoweza kuepuka kwa pande zote za wataalamu wa afya na wananchi,” amesema Mongella.


Kamati ya kuchunguza matukio hayo yaliyotokea Februari 26 na Machi 2, mwaka huu, iliongozwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Onesmo Rwakenderya.Kamati hiyo iliyoundwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magessa Mulongo iliwasilisha taarifa yake tangu Machi 7, mwaka huu, lakini haijaweza kutolewa hadharani.

google+

linkedin