Hii Hapa Barua ya SNURA ya Kuomba Radhi kwa Video yake ya Churaa | Yuvinusm

The Global News and Education

Breaking News
Loading...

5/5/16

Hii Hapa Barua ya SNURA ya Kuomba Radhi kwa Video yake ya Churaa

Baada ya serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutangaza rasmi jana kuifungia video ya Chura ya Msanii Snura Mushi, leo hii amejitokeza mbele ya Waandishi wa Habari na kuomba radhi umma wa Watanzania kwa kutengeneza video iliyomdhalilisha mwanamke.

Akitoa maelezo hayo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam Snura ambaye aliambatana na Meneja wake almaarufu kama HK ameiomba radhi serikali na Watanzania kwa kutengeneza, kuzindua na kuiweka mtandaoni video ya Chura isiyozingatia maadili ya Kitanzania.

“Mimi na Meneja wangu tunaomba radhi na tunaahidi kutorudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji na iwapo tutarudia tena basi tupewe adhabu kali kwa mujibu wa sheria za nchi” alisema Snura.

Katika hatua nyingine Snura amewataka wasanii wa muziki nchini kuhakikisha wanajisajili katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ili kazi zao ziweze kutambulika kisheria na tayari ameruhusiwa kufanya show katika majukwaa mbalimbali baada ya kujisajili katika baraza hilo na kupewa cheti.

IMG-20160505-WA0019 IMG-20160505-WA0022

google+

linkedin