5/18/16

Hii ndio siri ya wimbo ‘Yote Maisha’ ya Madee


Wimbo ‘Yote Maisha’ wa Madee ulikuwa wazo na P-Funk Majani aliyetaka uwe ujumbe kwa mzazi mwenzake, Kajala enzi hizo.
Kajala
“Kuna siku moja nilikuwa nachat naye [Kajala] halafu ngoma inapigwa kwenye TV fulani, nikamwambia angalia TV akakutana na hiyo nyimbo, nikamwambia hiyo nyimbo inakuhusu sana akasema ‘najua,” Madee alisema kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Mimi niliambiwa nifanye na Majani kwahiyo hisia hizo unazoziskia ni hisia za P-Funk.”
www.youtube.com/watch?v=7CBIwv8XgqE
Majani na Kajala wamewahi kuwa na uhusiano maarufu na wa muda muda mrefu uliowabariki mtoto wa kike, Paula. Huyo alikuwa mtoto wa pili wa producer huyo wa Bongo Records na wa kwanza kwa Kajala.
Hivi karibuni Madee aliachia video ya wimbo wake ‘Migulu Pande’ ambamo amemtumia Kajala.
Weka Maoni Yako Hapa
Share:

Advertisment

Habari Mpya

Follow us on Facebook

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © Yuvinusm | Powered by Blogger Design by Yuvinusm