5/29/16

Hip Hop na Waasisi wake Bongo

Unafahamika kama mziki wa kufokafoka ambao uliingia nchini mwanzoni mwa miaka ya 1990. Ulishika kasi kutokana na wasanii wengi kujaribu kufanya ubunifu katika mziki huo wakibadili mitindo kutoka Marekani na kufanya kwa maudhui ya kitanzania.
Huwezi kuutaja mziki huu ukawasahau wakongwe kama Mohamedy Balozi, Profesa Jay, Afande Sele, Jay Moe, Mr. II ama Sugu ambao walifanya kazi ya ziada kuiaminisha jamii kuwa mziki wa HipHop sio uhuni bali ni sehemu ya ajira kwa vijana.

Mziki huu ulizidi kufanya vizuri kutokana vijana wengi kuupenda na kuendelea kuufanya ambapo miaka ya 2000 uliendelezwa na Vijana kama Fid Q, Mwana FA, wakati AY na Joh Makini wao waliamua kufanya biashara kupitia HipHop ndipo wakatambulisha miondoko laini maarufu kama ‘HipHop Comercial’ na wamefanikiwa hadi sasa. Wakipewa nguvu na kituo cha Radio namba moja kwa vijana nchini Cloudsfm ambacho nacho kilikuwa kimeanzishwa miaka hiyo na kuwekeza kwenye mziki na vijana na kwa pamoja wamefanikiwa.

Hii leo tunazungumzia Walk it Off ya Fid Q ama Asanteni kwa kuja ya Mwana FA bila kusahau Don’t bother ya Joh Makini ni ngoma za Hiphop lakini zimefanywa kwa viwango vya kimataifa kuanzia mdundo hadi mashairi.Wakati Video ndio kabisa hazitii shaka hata kidogo hivyo inonesha kabisa kuwa njia iliyotengenezwa na Profesa Jay na wengine inaanza kuonyesha tobo leo. Kazi kwao kina Young Killer,Stamina na chipukizi wengine kuendeleza walipoishia wakongwe, japokuwa wapo wakongwe wengi ambao wanaweza kujifunza kutoka kwao.
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts