5/7/16

IFM yagomea Tuhuma Zake


Jengo la Chuo cha usimamizi wa fedha IFM dar es salaam

CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeeleza kufadhaishwa na habari zilizochapishwa na gazeti la Rai la tarehe 5 Mei mwaka huu Toleo la 1249 kuhusu utafunwaji wa mamilioni ya fedha kwenye chuo hicho.


Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Mkuu wa Chuo Kitengo cha Mipango, Fedha na Utawala inadai kwamba, taarifa hizo si za kweli.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba, Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaeleza kuwa, chuo hicho kilipokea fedha za ziada kutoka Wizara ya Fedha kwa ajili ya kulipa mishahara.

Inaeleza kuwa, pamoja na kupokea fedha hizo kutoka wizarani lakini walipaswa kuzirejesha ndani ya mwaka wa fedha 2015/2016 kama ripoti CAG ilivyoagiza katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Hata hivyo, taarifa hiyo inaeleza kuwa fedha hizo hawakuzitumia kwa kuwa, walifanikiwa kukusanya madeni kutoka kwa wanafunzi jambo ambalo liliwawezesha kutekeleza majukumu yao nje ya fedha hizo.

Fedha hizo walizikusanya kutoka Taasisi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na karo za wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/2015. Taarifa hiyo imeeleza kwamba, chuo hicho kinafanya kazi zake kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kuwa, kimekuwa kikipata hati safi kwa muda mrefu
Share:

Habari Mpya

Follow us Facebook

Popular Posts